Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Bi. Mwashabani Mrope amewataka Wanawake wa Wilaya ya Korogwe kujitokeza kwa wingi kuania nafasi mbalimbali za uongozi hasa tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu (2025) pia Wanawake mnapaswa kuchangamkia fursa za Mikopo ya Asilimia 10% inayotolewa na Halmashauri. Kauli hiyo aliitoa Bi. Mwashabani Mrope kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 05, 2025 kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Makuyuni iliyopo kata ya Makuyuni Wilaya ya Korogwe
Kwaupande mwingine Bi. Mwashabani Mrope alifafanunua kuwa Maadhimisho hayo yalete matokeo Chanya kwa kumwiinua Mwanamke kiuchumi na kuondokana na kasumba ya kuwa tegemezi katika Familia, Vilevile alieleza pawe na usawa wa Madaraka kati ya Wanaume na Wanawake kama kauli mbiu ya mwaka huu isemavyo “Wanawake, Wasichana 2025, Tuimarishe Haki,Usawa na Uwezeshaji”. Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kitaifa yanatarajia kufanyika Mkoani Arusha Machi 08, 2025 na katika Mkoa wa Tanga maadhimisho yanatarajia kufanyika Halmashauri ya Mji wa Handeni Machi 06 ,2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.