Afisa Tarafa ya Bungu Bw. Peter Kahindi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema amewataka wajane kujitokeza kwa wingi katika kumpigia kura Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025 kwa kutia tiki. Bw. Kahindi alitoa kauli hiyo kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Wajane na Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani yalyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Juni 23 (mwaka huu).
Naye Kaimu Mkurugenzi amabye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Happy Luteganya amesema kata zote 11 za Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni washirika kwenye Jukwaa la Wajane Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Majukwaa hayo yatasaidia kujiunua kiuchumi na kuondokana kuwa tegemezi katika Familia Jumla ya wajane waliohudhuria siku hiyo yapata Mia tatu na kumi (310).Kauli mbiu ya Siku hiyo inasema “Tuimarishe Fursa za Kiuchumi ,Kuchochea Maendeleo ya Wajane”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.