Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema amewataka Maafisa Ugani kuwafikia Wafugaji wote wanaojihusisha na Ufugaji ili kuondokana na changamoto ya magonjwa ya milipuko kwa Mifugo. Mh. Mwakilema ametoa kauli hiyo wakati wa Uzinduzi wa Chanjo za Mifugo katika Zizi la Mfugaji Mtaa wa Manzese Kata ya Kilole Julai 10, 2025.
Naye Mkuu wa Idara ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Ramadhani Sekija alieleza kuwa Halmashauri ya Mji wa Korogwe imepokea Jumla ya Chanjo 44,900 kutoka Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo Chanjo ya Ng’ombe ni 4000 Kwa ajili ya kutibu Homa ya Mapafu, Chanjo 900 kwa ajili ya Mbuzi na Chanjo 40,000 kwa ajili ya Kuku. Chanjo ya kuku hii inajulikana kama Tatu moja, ambayo inatibu Magonjwa matatu yakiwemo Mafua ya Kuku, Kideri na Ndui. Bw. Sekija alimwakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa watahakikisha kuwa Mifugo yote itachanjwa na kuwapatia Wafugaji Elimu ya kukabiliana na Magonjwa dhidi ya Mifugo yao. Ng’ombe wote watakaochanjwa watavalishwa hereni ili kutofautisha na Mifugo mingine.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.