Mwenyekiti wa kamati ya lishe Halmashauri ya Mji wa Korogwe aongoza kikao cha kamati ya lishe kwa robo ya kwanza July - Septemba 2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Novemba 18, 2025. Kaimu Mkurugenzi Dr. Miriam Cheche amesisitiza kuwa “wajumbe wa kamati ya lishe wahakikishe wanafanya kazi kwa pamoja kulingana na nafasi zao katika kamati ili kuzidi kupandisha ufanisi wa utekelezaji wa afua za lishe katika Halmashauri Mji wa Korogwe”.
Naye Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bw. Zabron Osima alitoa elimu juu ya utekelezaji wa afua za lishe pamoja na umuhimu wa lishe utoaji wa huduma za lishe kwa jamii unaolenga kuunga mkono Kauli mbiu ya lishe Afya ni mtaji wako zingatia unachokula.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.