Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Rashidi Kassim Mchatta ametaka maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi kanda ya Mashariki yaendane sambamba na mabadiliko ya takwimu zaidi kujikita katika uzalishaji. Bw. Mchatta ameyasema hayo Agosti 1, 2025 wakati akitembelea mabanda yaliyopo katika Mkoa Tanga hususani Banda la Korogwe Mji.
Ziara hiyo ya Bw. Mchatta ilipokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope, Maafisa Kilmo na Mifugo kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Katibu tawala Mchatta ameeleza kuridhishwa na ushirikiano wa Korogwe Mji na maandalizi yao yamefaa sana. Maonesho hayo kwa mwaka huu yanafanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkoani Morogoro kuanzia Agosti 1, hadi Agosti 8, 2025. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo ni Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Mizengo Pinda. Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane kwa mwaka huu 2025 yanasema “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.