Katibu Tawala Wilaya ya Korogwe atoa msaada Hospitali ya Lutindi
Kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ambapo kilele chake kitafanyika Desemba 9, mwka huu Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Bi. Rahel Mhando akiwa pamoja na Kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika Novemba 23, mwaka huu ameshiriki kazi za kijamii pamoja na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali katika Hospitali ya afya ya akili ya Lutindi iliyopo Kata ya Lutindi Wilayani Korogwe .
Maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika mwaka huu yanakwenda sambamba na utoaji wa misaada kwa makundi maalumu pamoja na kushiriki kazi mbalimbali za kijamii. Katika ziara ya kutembelea Hospitali ya Lutindi Bi. Rahel Mhando ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe akiwa pamoja na Kamati ya maaandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ameshiriki katika usafi wa mazingira pamoja na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kama vile mchele, unga wa sembe, sukari, mafuta ya kupikia pamoja na sabuni.
“Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika, serikali imeona ni jambo la busara kumipatia msaada ndugu zetu mliopo hapa ili tuweze kusheherekea kwa pamoja sikukuu ya uhuru wa nchi yetu” alisema Bi. Rahel Mhando ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya Korogwe wakati akitoa msada kwa wagojwa wa afya ya akili katika Hospitali ya Lutindi. Bi. Rahel alifafanua kuwa Serikali itaendeleza utamaduni wa kuwajulia hali wagonjwa waliopo Hospitali ya Lutindi ili kuwafariji katika kipindi kigumu wananchopitia.
“Natoa shukani kwa kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika na Serikali kwa ujumla kwa kutupatia msaada katika hosptitali yetu” alisema Dkt Marwa Katyetye ambaye ni mganga mkuu wa Hospitali ya afya ya akili ya Lutindi. Dkt Marwa alifafanua kuwa wagonjwa wa afya ya akili wanapotembelewa na ndugu, jamaa na marafiki wanapata faraja na kujiona pia ni sehemu ya jamii hivyo kupata uchangamfu wa akili.
Nae Mhe. Imanueli Mng’ong’oso ambaye ni Diwani wa Kata ya Lutindi alisema “ sisi wananchi tunaozunguka hospitali hii ya Lutindi, wagojwa wa afya ya akili waliopo Hospitalini hapa ni ndugu zetu bila ya kujali anatoka sehemu gani, wananchi wa Lutindi tunatoa shukrani za dhati kwa serikali kwa kuwapatia msaada ndugu zetu”.
Nao Wananchi wa Lutindi walioshirikia katika usafi wa mazingira pamoja na kuwajuli hali wagonjwa wakiambatana na Katibu wa Wilaya ya Korogwe walitoa shukrani kwa Viongozi wa Wilaya ya Korogwe na Serikali kwa ujumla kwa kutembelea Hospitali ya Lutindi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.