Mafunzo ya Vikundi 17 vilivyoidhinishiwa kupatiwa mikopo ya asilimia kumi yahitimishwa leo Agosti 15, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa Muda wa Siku tatu kuanzia Agosti 12 hadi yalipohitimishwa Agosti 15, 2025. Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ni Maafisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Afisa Biashara, Afisa Afya pamoja na Mkaguzi wa Ndani kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe.Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo wanakikundi juu ya usimamizi mzuri wa fedha ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.