Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda amemtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki Mh. Abubakar Kunenge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuongeza ubunifu kwenye Sekta za Kilmo, Mifugo na Uvuvi ili wakulima pamoja na Wafugaji wainuke kiuchumi.Mh Pinda alitoa kauli hiyo wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi (Nanenane) kanda ya Mashariki yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Agosti 2, 2025.
Katika Maonesho ya Nanenane Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni miongoni mwa Halmashauri 11 za Mkoa wa Tanga ambao unatekeleza kilimo cha Mazao ya Biashara na ya Chakula, Mazao ya Biashara yanayolimwa katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ni pamoja na Mkonge, Korosho, kwa upande wa mazao ya Chakula ni Mahindi na Mpunga. Maonesho ya Nanenane kanda ya Mashariki mwaka huu yanafanyika kuanzia Agosti 1, hadi Agosti 8, 2025 kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere yakiwa na Kauli mbiu inayosema”Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo, Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.