Mji wa Korogwe washiriki Kikao Kazi cha Maafisa Habari wa Serikali
Halmashaurri ya Mji wa Korogwe ikiwakilishwa na Afisa Habari wake Ndugu Jumanne Semagongo imeshiriki kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali. Kikao kazi hicho kimefunguliwa Mei 24 mwaka huu, na kitaendelea hadi Mei 28, Mkoani Mbeya katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mbeya cha Sayansi na Teknolojia (MUST) ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Lengo kuu la kikao kazi hicho ni kutoa mafunzo pamoja na kubadilishana ujuzi juu ya utoaji wa taarifa bora kwa Wananchi kuhusu Miraadi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikli. Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Utoaji taarifa kwa Umma ni Takwa la Kisheria, Viongozi wa Umma na Maafisa Habari tuwajibike”.
“Serikali tunatambua umuhimu wa Maafisa Habari Serikalini, tutaendelea kuwathamini” alisema Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi hicho cha Maafisa Habari wa Serikali. Nae Mhe. Puline Gekul ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alisemaa “Wanahabari tufanye kazi kwa bidii katika kumsaidi Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan”.
Kwa upande mwengine Ndugu Profesa Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pia alishiriki Kikao kazi cha Maafisa Habari wa Serikali kwa kuwa asilimia kubwa Maafisa Habari wa Serikali wanatoka kwenye Wizara yake. Ndugu Profesa Shemdoe wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi alitoa nasaha kwa Maafisa Habari wote wa Serikali kwa kuseama “ Maafisa wa Habari tangazeni miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali.”
Nao Maafisa wa Habati wa Serikali walioshirika kikao kazi cha mwaka huu Mkoani Mbeya waliishukuru Viongozi mbalilmbali wa Serikali kwa kushiriki ufunguzi wa Kikao kazi cha mwaka huu. Vilevile waliahidi kupokea pamoja na kufanyika kazi ushauri wote uliotolewa na Viongozi mbalimbali kwa lengo la kuboresha utoaji wa taarifa kwa Wananchi kuhusu Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.