Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Korogwe Bi. Mwashabani Mrope amewataka Wanamichezo ambao ni Watumishi wa Mji wa Korogwe wanaoshiriki Michezo hiyo kuwa na nidhamu katika kipindi chote cha Michezo kwani nidhamu ni kipimo cha utu. Bi. Mwashabani Mrope ameyasema hayo wakati akikabidhiwa Vifaa vya Michezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Korogwe Bw.Karim Awadh Seiph vyenye thamani ya Shilingi Laki Nne na Elfu Ishirini (420,000.00).Makabidhiano hayo yamefanyika Agosti 14, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Aidha kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sanaa, Utamaduni na Michezo Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Minael Mjema amesema jumla ya Washiriki wa Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) ni Thelathini na tano (35). Bi. Minael Mjema amemuahidi Mkurugenzi Timu zimejiandaa vizuri tangu mazoezi yalipoanza na tuko tayari kwa ushindi “alisema Mjema.”na kauli mbiu ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) inasema “Jitokeze kupiga kura kwa Maendeleo ya Michezo.”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.