Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe B. Mwashabani Mrope akiambatana pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo ametembelea Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo katika Sekta ya Elimu na Afya ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo inayofanywa na Serikali. Ziara hiyo imefanyika Julai 10, 2025 katika Maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Majengo,Ukarabati wa Soko la Manundu, Ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari Ngombezi, Ujenzi wa Nyumba ya Mganga Mfawidhi katika Zahanati ya Lwengera,Ujenzi wa Madarasa mawili ya Lanes katika Shule ya Msingi New – Korogwe, na Eneo maalumu la Ujenzi wa Shule mpya ya Msingi katika Shule ya Sekondari Joel Bendera.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.