Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh. William Mwakilema amewataka Madiwani kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kuimarisha na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri. Mapato yakikusanywa vizuri na kusimamiwa kwa uweledi mkubwa hakika Halmashauri itavuka lengo lililojiwekea. Mh. Mwakilema alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kinachohitimisha kipindi cha Robo ya Tatu katika Mwaka wa Fedha 2024/2025. Baraza hilo lilifanyika Mei 02, Mwaka huu (2025) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Mkurugenzi kushirikiana na Madiwani pamoja na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe tujitahidi kudhibiti miyanya ya upotevu wa mapato katika Halmashauri “alisema Mh. William Mwakilema ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe. Mh Mwakilema alifafanua kuwa mapato yakikusanywa kwa uadilifu na umakini itasaidia Halmashauri kujiendesha na kutekeleza miradi ya maendeleo kwani mapato ndiyo moyo wa Halmashauri.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mh. Francis Komba amesisitiza ukusanyaji wa Mapato ni jukumu letu sote kuanzia Madiwani pamoja na Wataalamu hivyo tuongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ili Halmashauri iweze kujiendesha yenyewe .
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.