Waziri wa Nchi Ofisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Mohamed Mchengerwa ametaka wanaosimamia Miradi ya TACTIC katika Miji 12 kuzingatia miktaba iliyosainiwa kwa mujibu wa Sheria pia amewaasa wakandarasi kufanya kazi kwa weledi. Mh. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa Hafla ya utiaji Saini Mikataba ya Utekelezaji wa Miradi ya Uboreshaji wa Miundo Mbinu ya Miji 12 Tanzania. Hafla hiyo imefanyika Juni 25, 2025 JijinI Dodoma.
Mh. Mchengerwa amesema miradi hiyo itaenda kuimarisha huduma za kiuchumi kwa Wananchi hususani upande wa mauzo na manunuzi kwa kuongeza thamani ya biashara Nchini amabapo Mazingira ya ufanyaji wa Biashara kwenye ngazi za Miji na Majiji yanenda kuboreshwa. Miradi hii yote itagharimu takribani Dola za Marekani Milioni 410 bila ya kodi ya ongezeko la thamani ya VAT ni mkopo wa mashart nafuu kutoka Benki ya Dunia.Miji itakayonufaika na mradi huo wa TACTIC Tanzania ni pamoja na Miji ya Morogoro, Songea, Tanga, Korogwe, Babati, Shinyanga, Bukoba, Bariadi, Lindi Iringa, Njombe na Manispaa ya Bukoba
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.