Shule ya Msingi Kwamngumi ni miongoni mwa Shule za Halmashauri ya Mji wa Korogwe inayotekeleza Elimu ya Kujitegemea (EK). Shule hiyo iko Kata ya Kilole inajihusisha na Kilimo cha Mahindi ili kuondokana na tatatizo la upungufu wa Chakula Shuleni. Shule hiyo imefanikisha kupanda jumla ya Hekari Mbili (2) za Mahindi aina ya Tumbili (Seed Co 555) ambayo itasaidia kutatua changamoto ya Wanafunzi ya kutokula Chakula Shuleni. Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Jumanne Feruzi alifafanua kuwa kupitia mavuno hayo yanayotarajiwa kuvunwa kipndi cha mavuno itachangia Wanafunzi kuhudhuria kwa wingi Masomo na kuinua kiwango cha Taaluma Shuleni. Nitoe wito kwa walimu wakuu wenzangu kuanzisha Kilimo cha kujitegemea Mashuleni ili kuondokana na changamoto ya Chakula Shuleni. Wanafunzi watanufaika kwa kunywa uji wakati wa Asubuhi pamoja na Chakula cha Mchana. Mwalimu mkuu Feruzi alitoa ufafanuzi huo Juni 19, 2025 katika Shamba la Shule lilioko kwamngumi Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.