Tanzania yaungana na Nchi zingine za Afrika Kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ikiwa na lengo la kuwakumbuka Watoto waliouawa kwenye maandamano ya Wanafunzi ikiwa ni kupinga mfumo wa Elimu ya kibaguzi ilikuwa inatolewa na Utawala wa Afrika ya Kusuni. Mauaji hayo ya Watoto takribani 2,000 yalifanywa na Utawala wa Makaburu Afrika kusini Mnamo Tarehe 16 Juni, 1976. Ilipofika Mwaka 1991 Umoja wa Nchi huru za Afrika zilifanya maamuzi ya kuwaenzi Watoto hao. Kaulimbiu ya Mwaka huu ya Siku ya Mtoto wa Afrika ni “Haki za Mtoto Tulipotoka, Tulipo na Tuendako.”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.