TARURA yatenga Shilingi Bilioni 1.8 ujenzi wa barabara Mji wa Korogwe
Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Wilaya ya Korogwe (TARURA) katika Mwaka wa fedha 2023/24 imetenga Bajeti ya Shilingi Bilioni 1.8 {Tsh. 1,889,600,000} kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara zenye urefu wa Kilomita 48.3 katika Mji wa Korogwe. Bajeti hiyo ilitangazwa wakati wa Kikao cha Madiwani kilichofanyika Februari 03, Mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“ Katika mwaka wa fedha 2023/24 TARURA imejipanga vyema kufungu mtandao wa Barabara za Mji wa Korogwe katika kiwango cha Lami, Changarawe pamoja na Ujenzi wa Madaraja” alisema Bw. Godfrey Bwire ambaye ni Meneja wa TARURA Wilaya ya Korogwe. Bw. Bwire alifafanua kuwa Ujenzi wa Barabara hizo zitashusisha Barabara zilizopo katikati ya Mji pamoja na Barabara zilizopo pembeni ya Mji wa Korogwe.
“Natoa pongezi kwa TARURA kwa maandalizi mazuri ya Bajeti, Bajeti yao imegusa kila maeneo ya Mji wa Korogwe” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mhe. Komba alifafanua kuwa uboreshaji wa Barabara katika Mji wa Korogwe kutasaidia kuvutia Wawekezaji na kuufanya Mji wa Korogwe kuimarika kiuchumi.
Nae Bw. Charles Salu ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilya ya Korogwe Mji alitoa pongezi kwa maendeleo mazuri ya Ujenzi wa Barabara katika Mji wa Korogwe kwa kusema “pamoja na mtikisiko wa uchumi Duniani, Mama ( Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan) ameendelea kutoa fedha za Ujenzi wa Barabara. Chama cha Mapinduzi na Wananchi kwa ujumla tunampongeza sana”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.