Vikundi 17 vilivyoidhinishiwa kupatiwa mikopo ya Asilimia kumi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe vimepatiwa mafunzo ya jinsi ya usimamizi mzuri wa fedha katika vikundi vyao ili vikundi hivyo viweze kutimiza lengo la kuwakomboa Wananchi kiuchumi. Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni Maafisa wa maendeleo ya Jamii wa Mji wa Korogwe pamoja na Maafisa Kilimo, Mifugo na Mchumi kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mafunzo hayo yalifanyika Agosti 13, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na yatahitimishwa Agosti 15, 2025.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.