Afisa Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bi. Sharifa Wanja amewataka Waratibu Elimu kata pamoja na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Kwenda kuunda Timu ya Ufuatiliaji wa Dhima, Dira na Misingi bora ya uendeshaji wa Shule zetu. Bi. Sharifa Wanja ameyasema hayo kwenye kufunga Mafunzo ya Jumuiya za Kujifunza (JZK). Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa muda wa Siku mbili kuanzia Juni 26, 2025 na kuhitimishwa Juni 27, 2025. Mafunzo hayo yalifungwa rasmi Juni 27, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Msingi New Korogwe.
Lengo kuu la Mafunzo ni kuwajengea uwezo Viongozi katika usimamizi wa Ujifunzaji na Ufundishaji kwa Maafisa Elimu ngazi ya Halmashauri , Maafisa Elimu kata pamoja na Walimu wakuu wa Shule zote za Msingi zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Sambamba na ufungaji wa Mafunzo ya Jumuiya za Kujifunza (JZK) Bi. Sharifa Wanja alitoa Tathmini ya Matokeo ya Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Nne na Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi wa Darasala Saba k wa Mwaka 2024. Afisa Elimu Msingi alifafanua kuwa Halmashauri ya Mji wa Korogwe imeingia Kumi Bora kitaifa kwa Matokeo mazuri ya Darasa la saba kwa Mwaka 2024 na kupata Tuzo, hivyo akawaomba Waratibu na Walimu wakuu kuwasimamia Walimu katika ufundishaji ili tusilewe sifa , nao Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Korogwe Mjini haikuwa nyuma katika Pongezi hizo, wakatoa Cheti cha Pongezi kwa Bi. Sharifa Wanja ambaye ni Afisa Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.