Brac Tanzania yatoa msada katika Mji wa Korogwe
Taasisi ya Brac Tanzania imetoa msada wa vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya Shule zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ikiwa ni jitihada ya kuiunga mkono Serikali katika ya mapambano ya ugonjwa wa Corona (Covid - 19).
Vifaa vilivyotolewa na Taasisi hiyo vina thamani ya Shilingi milioni mbili, laki mbili na elfu ishirini. Vifaa hivyo ni pamoja na matanki kumi na mbili (12) yaliyofungwa kwenye meza maalumu pamoja na vitakasa mikono (sanitaiza). Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika Julai 17, mwaka huu katika ofisi za Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungunzia msada huo Mkurugenzi wa Brac Tanzania Ndugu Kafwew Fordison alisema “tumeguswa na jitihada ya Serikali katika mapambano ya ugonjwa wa Corona (Covid - 19) na sisi tumeona ni muda muafaka kuungana na jitihada hizi kwa kutoa vifaa vya kunawia mikono katika shule”. Ndugu Fordison alifafanua kuwa msada huo waliotoa ni muendelezo wa ugawaji wa vifaa vya kunawia mikono kwaajili ya shule zilizopo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Nae Dr. Fortunata Silayo anayemuakailisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “tunatoa shukrani kwa Taasisi ya Brac Tanzania kwa kutupatia vifaa vya kunawia mikono katika shule zetu ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid - 19).
Kwa upande mwingine Ndugu Kasimu Kaoneka ambae ni Afisa Elimu Shule za Msingi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “vifaa mlivyotupatia vitasaidia katika mapambano ya ugonjwa wa Corona (Covid – 19) na vilevile kuwa sehemu ya somo la usafisishaji wa mikono kwa wanafunzi”. Ndugu Kaoneka alifafanua kuwa vifaa hivi vitagaiwa katika shule za msingi takribani kumi na mbili.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.