Halmashauri ya Mji wa Korogwe yaadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imeadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani, maadhimisho ambayo hufanyika Oktoba 11, ya kila mwaka. Kwa mwaka huu maadhimisho haya yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ambapo mgeni rasmi alikuwa Mh. Francis Komba diwani wa Kata ya Mtonga ambapo pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Maadhimisho haya yaliandaliwa na taasisi ya Brac Tanzania na kuhudhuriwa pia na watoto wa kike kutoka takribani shule za sekondari kumi na moja za Mji wa Korogwe. Lengo la maadhimisho haya ni kukukutanisha wanaharakati mbalimbali ambapo huelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu maswala ya mtoto wa kike duniani. Kauli mbie ya mwaka huu ni “ imarisha uwezo wa mtoto wa kike: tokomeza ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni”.
Kwa upande wa mgeni rasmi Mh. Komba amewataka watoto wa kike kuongeza bidii katika masomo. Alisistiza kuwa mtoto wa kike akipata elimu ataweza kujitambua na kuepukana na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumrudisha nyuma kimaendeleo. Nae Bwana Aseri Mshana ambaye ni afisa elimu ya watu wazima akatika Halmashauri ya Mji wa Korogwe amewataka watoto kwa kike kujiepusha na vishawishi vya kimapenzi kwani wanaweza kupata madhara kama vile mimba za utotoni pamoja na maradhi ya ukimwi.
Katika hatua nyingine Mackleo Sumra mwanafunzi kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Korogwe alisema maadhimisho haya ni muhimu sana kwa mtoto wa kike kwani wamepata maarifa yakutosha ambayo yatawasaida kuweka mikakati ili kufikiakia maengo ya kielimu na maisha kwa ujumla. Nae afisa habari wa Brac Tanzania ndugu Jackline Christopher ambao ni waandaaji wa maadhimisho haya alisema amefurahishwa na ushiriki wa watoto wa kike kutoka shule mbalimbali za sekondari hivyo watasaidia kufikisha ujumbe kwa watoto wengine katika jamii.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.