Halmashauri ya Mji wa Korogwe yatoa mafunzo ya kisheria kwa mabaraza ya Kata
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imetoa mafunzo ya kisheia kwa mabaraza kumi na moja ya kata kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kisheria ili kupunguza migogoro ya kisheria inazojitokeza katika jamii. Mafunzo haya ya siku tatu yalifunguliwa Oktoba 2, mwaka huu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauriya Mji wa Korogwe Ndugu Nicodemus Bei katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzia mafunzo haya mwanasheria msaidizi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Ndugu Mussa Dotti alisema mafunzo haya yapo kisheria katika sheria ya mabaraza ya Kata sura 206 rejeo la 2002, hivyo wameandaa mafunzo haya ili kuwajengea uwezo mabaraza ya kata katika kutatua migogoro na kutoa ushauri wa kisheria katika maeneo wanayoishi. Bwana Dotti alifafanua kuwa maeneo makuu yanayohitaji utatuzi wa kisheria ni ardhi na kesi ndogondogo katika jamii.
Kwa upande mwingine Bi. Susana Joseph ambaye pia ni mwanasheria msaidizi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema katika siku za karibuni kumeongezeka migogoro mingi ya ardhi katika jamii hivyo mafunzo haya ya kisheria kwa mabaraza ya kata yatasaidia pupunguza changamoto za ardhi zinazojitokeza.
Nae Bwana Afred Dege ambaye ni mshiriki wa mafunzo haya kutoka kata ya Magunga alisema mafunzo haya ya kisheria yatawasaidia kutatua migogoro na kutoa ushauri wa kisheria katika jamii kwa sababu walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea . Pia Bi. Felista Nyonjele mshiriki kutoka Kata ya Manundu ameishukuru Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kuandaa mafunzo haya ya kisheria na elimu waliyoipata itawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.