Hospitali ya Mji wa Korogwe yapata mashine mpya ya x-ray
Wizara ya Afya imeipatia Halmashauri ya Mji wa Korogwe mashine mpya ya mionzi (x-ray) kwaajili ya Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga) ikiwa ni mkakati wa Serikali katika uboreshaji wa huduma za afya. Mashine hiyo imeanza kutoa huduma rasmi kuanzia Agosti 24, mwaka huu.
Akizungumzia mchakato wa mashine hiyo, Ndugu Nicodemus Bei ambaye ni Mkurugenzi waHalmashauri ya wa Mji wa Korogwe alisema “huduma za mionzi katika Hosptitali yetu ya Mji wa Korogwe tumeziboresha, wananchi wa Korogwe na Watanzania kwa ujumla tutawapatia huduma bora na kwaharaka zaidi”. Ndugu Bei aliendelea kufafanua kuwa mashine hiyo ni ya kisasa ina thamani ya Shilingi Milioni Mia Mbili.
Nae Dr. Elizabeth Nyema ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema “tunatoa shukrani kwa Wizara ya Afya kwa kutupatia mashine mpya ambayo itasaidia kupunguza tatizo la huduma za mionzi katika hospitali yetu”. Dr. Nyema alisisitiza kuwa huduma za mionzi zitaendelea kutolewa kwa saa ishirini na nne na siku saba za wiki.
Kwa upande wa Dr. Heri Kilwale ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Korogwe (Magunga) alisema “wataalamu wetu wa huduma za mionzi wamejipanga vyema katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi ili kuhakikiasha Serikali inafikia lengo lake” Kwa upande wa wagonjwa waliopatiwa huduma ya mionzi baada ya mashine hiyo kuzinduliwa walisema “tunafuraha kubwa kwa kupatiwa huduma ya mionzi yenye uhakika na kwa haraka zaidi”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.