Akiongea katika uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa shule ya Sekondari Ngombezi jana 03/07/2019, Ndg . Mzee Mkongea Ally aliwaagiza viongozi na watumishi wa umma kupinga rushwa ili kila mwananchi aweze kupata haki zake.Lengo la kuanzishwa kwa klabu hiyo shuleni hapo ni kuwajengea wanafunzi weledi wa namna ya kupinga rushwa hata watakapokuwa raiya au watumishi wa umma baadaye.
Pia katika tukio lingine kiongozi huyo alizindua ujenzi wa mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 160 ambayo hadi sasa yapo katika hatua za mwisho na yameshagharimu jumla ya Tsh 141,943,072 na nguvu za wananchi zinazofikia Tsh 3400,000.
Aidha mradi mwingine uliozinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi ni mradi wa maji katika eneo la Manzese utakaonufaisha wananchi waishio Kwamngumi,Manzese na Kambi ya maziwa ambapo hadi ukamilike utagharimu kiasi cha Tsh 219,674,660.
Hatahivyo mbio za Mwenge wa Uhuru zilitembelea mradi wa kikundi cha Baraka-Vijana kinachojihusisha na utengenezaji wa samani za ndani (furniture) kata ya Kilole.Pia ulitembelea Mnara wa makumbusho ya Mwalimu Nyerere uliopo eneo la Alamkhan Old Korogwe.
Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka nchini kote kwa ajili ya kuibua ari ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzindua, kutembelea na kufungua miradi mbalibali inayotekelezwa na serekali.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.