Kituo cha afya Majengo chaanza upasuaji
Kituo cha afya Majengo katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe kimeanza kutoa huduma za upasuaji huduma ambazo zilikuwa sikisubiriwa kwa muda mrefu. Kwa mara ya kwanza upasuaji wa dharura wa mama mjamzito umefanyika Oktoba 16, mwaka huu katika chumba maalumu cha upasuaji kilichopo kituoni hapo.
Akizungumzia upasuaji huu, Dr. Kelvin Samike kiongozi wa jopo la madaktari alisema upasuaji ulifanywa na madaktari watatu wakisaidiwa na muuguzi mmoja pamoja na mtaalamu wa usingizi. Dr. Samike aliendelea kusema kuwa walifanikisha vyema upasuaji na mjamzito alibahatika kupata mtoto wa kike. Kwa upande wa ndugu Leonard ambaye ni mtaalamu wa usingizi alisema kazi ya upasuaji ilifanywa kwa ufanisi mkubwa na kila kitu kilikwenda vyema.
Nae Easter Ugomba ambaye ni muuguzi aliyeshiriki katika mchakato wa upasuaji alifafanua kuwa upasuaji ulikwenda vizuri. Baada ya upasuaji kukamilika mama na mtoto waliwapatia kitanda wakiwa chini ya uangalizi wa madaktari na baada ya saa 24 kuona hali ya mama na mtoto imeimarika vyema waliwaruhusu kwenda nyumbani.
Kwa upande mwingine Dr. Elizabeth Nyema ambae ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema anafuraha kubwa kuona kwa sasa Kituo cha afya Majengo kinatoa huduma za upasuaji. Dr Nyema aliongeza kusema kuwa haya ni matunda baada ya kupata fedha za ukarabati kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Hata hivyo alisisitiza kuwa licha ya kuwa na huduma za upasuaji pia wanazo huduma nyingi nzuri kituoni hapo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.