Korogwe Girls 1996 Group yachangia mifuko mia moja ya saruji ujenzi wa ukuta shule ya sekondari ya wasichana korogwe
Kikundi chenye wanafunzi thelathini waliomaliza shule ya sekondari ya wasichana korogwe mwaka 1996 wametoa ahadi ya kuchangia mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ukuta katika shule ya sekondari ya wasichana Korogwe. Ahadi hii imetolewa Oktoba 13, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano uliopo shuleni hapo.
Ndugu Janine Mallya ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi cha Korogwe Girls 1996 Group alitoa ahadi hii walipotembelea shuleni hapo kwa lengo la kumuenzi kwa vitendo Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere akiwa anatimiza miaka 20 tokea atutoke duniani. Sambamba na kumuenzi baba wa taifa pia wamekuja kusisitiza umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla. Pamoja na kutoa ahadi ya saruji pia walikabidhi taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na uzalendo kwa shule yao waliyosoma.
Nae Mwl. Mercy Kitali akimuwakilisha Mkuu wa shule alishukuru kwa ahadi ya kutolewa mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ukuta pamoja na kupokea taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi. Alisema ni jambo la faraja sana kwa ujio wa ugeni huu, ujio wao umetoa hamasa kubwa kwa watoto wa kike waliopo hapa shuleni kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao ya kuelimu na maisha kwa ujumla. Pia amefurahi kuona wanafunzi aliowafundisha kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, makampuni binafsi na wengine kuwa wajasiriamali wakubwa hapa nchini.
Kwa upande mwingine Bi. Anjela Nyaki ambaye ni mwanakikundi cha Korogwe Girls 1996 Group na kwa sasa ni mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro aliwasisitizia wanafunzi ili kufikia malengo yao kielimu na kimaisha kwa ujumla ni muhimu kuwa na nidhamu, kufanya ibada kila wakati pamoja na kusoma kwa bidii. Nae Mwanafunzi Jackline Amosi amefurahi kuona wanafunzi walisoma katika shule yao wamefanikiwa kuwa wataalamu wa fani mbalimbali na wao watasoma kwa bidii ili kupata mafanikio kama yao.
Wakati wa kuagana Bi. Anna Shanalingiwa ambaye ni katibu wa kikundi cha Korogwe Grils 1996 Group alifafanua kuwa ujiwa wao hapo shuleni ni mwanzo naitakua muendelezo kwa siku nyingine hata hivyo amefungua milango kwa mwanafunzi yoyote aliyemaliza shule ya sekondari ya wasichana korogwe na anauzalendo wa shule yake anaweza kuwatafuta kwa ajili ya kuchangia fedha au ushauri kwa ajili ya maendeleo ya shule hii kupitia nambari +255758172939.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.