Madiwani wa Mji wa Korogwe kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa madeni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Francis Komba amewataka Madiwani wote wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa madeni kwenye Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ambao walikopeshwa na Halmashauri na fedha hizo hawajerejesha kwa muda mrefu.
Mwenyekiti ametoa agizo hilo wakati wa Baraza la Madiwani la Papo kwa Papo la Robo ya Nne kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 lililofanyika Agosti 5, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Madiwani katika kila Kata nendeni mkasimamie ukusanyaji wa fedha kwenye vikundi vilivyokopa na havijarejesha fedha hizo”alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Mhe. Komba alifafanua kuwa fedha zinazodaiwa kwenye vikundi zitakaporejeshwa zitasaidi kukopeshwa vikundi vyengine ili nao waweze kunufaika na mikopo ya Halmashauri.
“Halmashauri tutaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo mpaka tutakapohakikisha tumefikia malengo tuliyojiwekea” alisema Ndugu Nicodemus Bei ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa Baraza hilo la Madiwani la Papo kwa Papo. Ndugu Bei alifafanua kuwa kwa sasa Halmashauri inaendelea na utekelezaji wa miradi ya Elimu na Afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma karibu na maeneo yao.
Kwa upande mwengine, Madiwani nao waliwasilisha taarifa za Kata zao wakiainisha mafanikio pamoja na changamoto zilizopo katika jamii zinazoitaji utatuzi. Nae Ndugu Fulgence Komba ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mji Mhe Dr. Alfred Kimea alisema “nimefurahishwa na taarifa za Madiwani, taarifa zao ziko wazi na zenye kuleta matumaini kwa Wananchi” Ndugu Komba alisisitiza kuwa taarifa hizo za Madiwani zitasidia kuwa dira kwa Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugezi pamoja na Mbunge katika kutatua kero za Wananchi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.