Mh. Zena Said Katibu Tawala Mkoa wa Tanga ashiriki mashindano ya mbio fupi za Korogwe “ Korogwe Min Marathon”
Mh. Zena said amefungua pamoja na kushiriki mashindano ya mbio fupi za korogwe maarufu kama Korogwe Min Marathon. Mashingano ambayo yalifunguliwa Oktoba 13, mwaka huu katika eneo la kiwanja cha Chuo cha Ualimu Korogwe kikijulikana kama Korogwe TTC.
Mh. Zena ambaye ni mgeni rasmi katika mashindano alisema lengo kuu la mashindano haya ni umuenzi kwa vitendo Baba wa Taifa Mwl. J.K.Nyerere ikiwa mwaka huu ametimiza miaka 20 tokea atutoke duniani . Pamoja na kumuenzi baba wa Taifa vilivile kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za wilaya ya Korogwe.
Kwa upande mwingine Mh. Zena amewataka wananchi wa Korogwe kwenda kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili wachague viongozi makini watakaowaletea maendeleo katika maeneo yao. Sambamba na mashindano pia amewatembele walimu tarajali wa chuo cha ualimu Korogwe na kuwasisitiza umuhimu wa kujiandikisha ili washiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu.
Mh. Zena akiwa pamoja na mwenyeji wake Mh. Kissagwakisa Kasongwa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Korogwe wote kwa pamoja walishiriki katika mbio fupi za kilometa 5 mbio hizi zikiwa na lengo la kujifurahisha na kuuchangamsha mwili. Nae mratibu wa mashindano haya ndugu Juma Mwajasho alisema mashindano yamegawanyika katika vipengele vifuatavyo mbio za miguu kilometa 5 kwa ajili ya kujifurahisha, kilometa 10 mashindano ya wasichana na wavulana. Vilevile mbio za baiskeli kilometa 20 kwa wasichana na kilometa 30 kwa wavulana.
Nae Banuelia Braiton kutoka Mkoani Kilimanjaro ambaye ni mshindi wa pili wa mbio za kilomita 10 kwa wasicha amefurahi kupata ushindi na ameshauri mashindano haya yasiishie mwaka huu yawe endelevu kwa miaka mingine. Akizungumzia kuhusu fursa zilizopo katika michezo amesisitiza kuwa wakati huu michezi ni ajira hivyo vijana washiriki kwa wingi, ushiriki wao utasaidi kupata fedha pamoja na kuimarisha mwili.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.