Halmashauri ya Mji wa Korogwe katika mwaka wa fedha 2021/2022 imepanga kukamilisha ujenzi wa zahanati mbili ili kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa mji wa Korogwe. Ujenzi wa Zahanati hizo utakaogharimu takribani Shilingi Milioni Mia Moja na Hamsini unajumuisha zahanati ya Kitifu iliyopo Kata ya Mgombezi pamoja na zahanati ya Kilole iliyopo Kata ya Kilole.
Mkakati wa ujenzi wa zahanati hizo ulitolewa katika Baraza la Madiwani la maswali ya hapo kwa hapo lililofanyika Aprili 29, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Wataalamu mtusaidie kutatua changamoto cha miundominu katika Mji wa Korogwe” alisema Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Diwani wa Kata ya Mtonga wakati akitoa nasaha kwa Wataalamu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Taasisi nyingine za Serikali zenye jukumu la kutoa huduma za jamii wakati wa Baraza la Madiwani la maswali ya hapo kwa hapo.
Kwa upande mwingine, Bi. Bernadetha January ambaye ni Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi alisema “katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri tutahakikisha tunakamilisha ujenzi wa zahanati za Kitifu na Kilole ili wanachi wapate huduma za afya kwa karibu”. Nae Bi. Jamila Bakari ambaye ni Mwananchi wa Mji wa Korogwe aliyehudhuria kwenye Baraza la Madiwani la maswali ya hapo kwa hapo alisema “iwapo Serikali itakamilisha ujenzi wa zahanati mbili ilizoziahidi itasaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi ”.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.