Mji wa Korogwe wapitisha bajeti ya mwaka 2021/2022
Halmashauri ya mji wa Korogwe katika mwaka wa fedha 2021/2022 imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Bilioni Ishirini. Taarifa hiyo ya bajeti ilitolewa kupita kikao cha madiwani cha bajeti kilichofanyika Februari 3, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Tuhakikishe tunathibiti uvujaji wa mapato ya Halmashauri” alisema Mhe. Fransic Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Diwani wa Kata ya Mtonga wakati akipokea taarifa ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Mhe. Komba alisisitiza kwa kusema “Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalamu ni vyema tukashirikiana kwa pamoja katika kuibua vyanzo vipya vya mapato katika Halmashauri yetu”.
“Mpango huu wa bajeti umeshirikisha wananchi kuanzia ngazi za Mitaa, Vijiji hadi Kata” alisema Ndugu Nicodemus Bei ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mpango wa bajeti kwa mwaka 2021/2022. Ndugu Bei aliendelea kufanua kuwa mpango huo wa bajeti unalenga zaidi kuwashirikisha wananchi katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini.
Kwa upande mwengine, Ndugu Emanuel Chale ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Korogwe Mjini alitoa pongezi kwa Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi pamoja na Wataalamu wa Halmashauri kwa maandalizi mazuri ya bajeti hususani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.