Mji wa Korogwe washinda Vikombe Saba UMISSETA
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imepata ushindi wa kishindo kwa kupata Vikombe Saba katika mashindano ya Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA). Mashindano hayo yaliyoshirikisha Halmashauri zote Kumi na Moja za Mkoa wa Tanga yalifanyika kuanzia Juni 11 hadi 13, mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga iliypo Tanga Mjini.
Katika mashindano hayo Halmashauri ya Mji wa Korogwe ilipata Vikombe Saba ambapo Vikombe Sita imeshika nafasi ya Kwanza na Kikombe kimoja imeshika nafasi ya Pili. Michezo iliyoshindaniwa katika mashindano hayo ilijumuisha Mpira wa Miguu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Wavu pamoja na Mpira wa Pete. Michezo mingine ni Mpira wa Kikapu, Mchezo wa Riadha pamoja na Uimbaji wa Nyimbo (Kwaya).
“Natoa pongezi kwa Wanafunzi wote waliotupatia ushindi katika michezo ya UMISSETA” alisema Mwl. Salim Makame ambaye ni Mwalimu wa Michezo kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe aliyeambatana na Wanafunzi katika mashindano hayo. Mwl. Makame alifafanua zaidi kuwa wanafunzi 31 kati ya Wanafunzi 79 wamechaguliwa kuunda Timu ya UMISSETA ya Mkoa Tanga itakayoshiriki katika mashindano ya Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Mtwara.
Kwa upande mwingine, Wanafunzi 48 waliwasili Mjini Korogwe baada ya mashindano ya UMISSETA Mkoani Tanga kukamilika walitoa pongezi kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa kuwapa ushirikiano wa kutoasha uliopelekea ushindi wa Vikombe Saba.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.