Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe atembelea miradi ya maendeleo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe pamoja na Wakuu wa Idara, na Vitengo wametembelea miradi ya maendeleo ya elimu inayotekelezwa na Serikali ya wamu ya Tano chini ya Mh. Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo. Ukaguzi huo wa miradi umefanyika Agosti 25, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Korogwe.
Miradi hiyo ya uboreshaji wa elimu inaojulikana kama EP4R awamu ya nane ina thamani ya takribani Shilingi Milioni Mia Tisa. Ambapo utekelezaji wake unahusisha ujenzi wa miundombinu katika shule za Msingi kumi na moja pamoja na Shule tatu za Sekondari. Shule za Msingi ni pamoja na Manundu, Mbeza, Majengo, Boma, Zung’nat, Magunga, Kwasemangube, Kwamndolwa, Kilole, Kwamsisi na Msambiazi. Kwa upande wa Shule za Sekondari ni pamoja na Shule ya Wasichana ya Korogwe, Semkiwa pamoja na Kimweri.
Akizungumzia miradi hiyo Bi. Benadetha January ambaye ni Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe akimuakilisha Mkurugezi alisema “miradi ya elimu tunayoitekeleza katika mwaka wa fedha 2020/2021 inahusisha ujenzi wa madarasa, mabweni pamoja na matundu ya vyoo”. Bi. January alifafanua kuwa miradi hiyo ikikamilika itasaidia kupunguza changamoto zilizopo katika shule za Msingi pamoja na Sekondari.
Nae Mhandisi Said Abuu pamoja na Mhandisi Fredy Mkondya ambao ni wahandisi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na ndio wasimamizi wa miradi hiyo walisema “miradi yote ya ujenzi wa madarasa, mabweni na matundu ya vyoo inakwenda vyema” Mhandisi Abuu alisisitiza kuwa mpaka kufikia mwezi Novemba mwaka huu miradi yote itakua imekamilika.
Kwa upande wa Afisa Elimu Sekondari Bi. Uria Ndelwa pamoja na Afisa Elimu Msingi Ndugu Kasimu Kaoneka walisema “miradi hii ya elimu itakapokamilika itasaidia kuboresha mazingira mazuri ya ufundishaji na kuchangia ongezeko la ufaulu katika shule zetu”
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.