Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe atembelea miradi ya maendeleo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe akiambatana pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali ametembelea miradi ya maendeleo iliyopo katika Mji wa Korogwe inayotekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2020/2021. Ziara ya miradi hiyo imefanyika Oktoba 22, mwaka huu.
“miradi hii ya elimu pamoja na afya itakapokamilika itasaidia kupunguza baadhi ya changamoto katika halmashauri yetu” Dr. Furtunata Silayo ambaye ni Afisa Mifungo na Uvuvi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemuwakilisha Mkurugenzi alisema.. Dr. Silayo alisisitiza kuwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inaboresha huduma za jamii pamoja na kuwapatia mikopo vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na vikundi kwa ujumla.
Nae Bi. Benadetha January ambaye ni Mchumi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe alifafanua kuwa miradi iliyotembelewa inahusisha Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa pamoja na Matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari, Ujenzi wa Mabweni katika Shule za Sekondari, Ujenzi wa vyoo vya kisasa katika Soko la Manundu, pamoja na Vikundi vya Vijana,Wanawake na Watu wenye ulemavu. Miradi mingine ni Ujenzi wa vyumba vya kulalia wagonjwa pamoja na Mtambo wa kuchomea taka katika Kituo cha Afya cha Majengo.
Kwa upande mwingine Wakuu wa Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari, Afya pamoja na Maendeleo ya Jamii wameridhishwa na maendeleo mazuri ya utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo. “nitahakikisha miradi yote ya ujenzi inakamilika vyema ikiwa katika viwango vilivyotolewa na Serikali.” Mhandisi Said Abuu alisisitiza wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ubora wa malighafi zilizotumika katika ujenzi wa miundombinu ya elimu pamoja na afya.. Nae Bi. Jane Steven kutoka kikundi cha Agape kinachojihusisha na utengenezaji wa batiki pamoja na mapambo malimbali aliishukuru serikali na Halmashauri kwa ujumla kwa kuwapatia mkopo katika kikundi chao.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.