Mkuu wa Mkoa wa Tanga apigia chapuo kilimo cha mkonge
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima amewaagiza Maafisa Kilimo wa Halmashauri za Wilaya ya Korogwe kuongeza uzalishaji wa kilimo cha mkonge ikiwa ni mkakati wa Serikali katika kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Tanga na Nchini kwa ujumla. Agizo hilo amelitoa wakati wa Baraza la Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019 / 2020 lililofanyika Juni 17, mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
“Tunataka kurudisha hadhi ya Mkoa wa Tanga katika kilimo cha mkonge” alisema Mhe. Adam Malima ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga wakati akitoa maagizo kwa Maafisa Kilimo wa Halmashauri za Wilaya ya Korogwe katika kikao cha Baraza la Hoja za Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019 / 2020. Mhe. Malima aliendelea kutoa maelekezo kwa kusema “Wilaya ya Korogwe hakikisheni mnaongeza uzalishaji wa mkonge kutoka tani elfu tisa hadi tani elfu thelathini kwa mwaka”.
“Niko tayari kwa utekelezaji wa maagizo ya kilimo cha mkonge” alisema Ndugu Ramadhani Sekija ambaye ni Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati akipokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kuhusu kuongeza uzalishaji wa kilimo cha mkonge katika Wilaya ya Korogwe wakati wa Baraza la Hoja za Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2029 / 2020.
Katika hatua nyengine, Mhe. Adamu Malima ameipongeza Halmashauri ya Mji wa korogwe kwa uandaaji pamoja na uwasilishaji mzuri wa taarifa za Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019 / 2020. Nae Mhe. Francis Komba ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Diwani wa Kata ya Mtonga alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa kuitembelea Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.