Mkuu wa Wilaya ya Korogwe azindua Kampeni ya Bima ya CHF
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Alexander Mhando amezindua Kampeni ya undikishaji wa Wananchi katika Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa kwa wakazi wa Mji wa Korogwe. Kampeni hiyo imezinduliwa Juni 24, Mwaka huu katika Viwanja vya Soko la Manundu.
“Tuendelee kujiunga katika mfuko wa bima ya afya ya jamii kwa faida yetu” alisema Mhe. Alexander Mhando wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uandikishaji wa Wananchi katika Bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa. Mhe. Mhando alifafanua kuwa itakuwa vizuri zaidi kila Mwananchi atayejiunga kwenye Bima ya Afya ya CHF akawe balozi kwa Wananchi wengine ili nao waweze kunufaika na Bima hiyo.
“Wananchi tujiunge kwa wingi katika bima ya CHF, hii bima gharama zake ni nafuu ukilinganisha na bima nyingine” alisema Bi. Charity Sichona ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe anayemuwakilisha Mkurugenzi katika Uzinduzi wa Kampeni ya Bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa.
Nae Mratibu wa Bima ya Afya ya CHF katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe Ndugu Judith Kazimoto alifafanua kuwa gharama za kujiandikisha katika Bima ya Afya ya CHF kwa Kaya Moja ni Shilingi Elfu Thelathini kwa Mwaka na Kaya Moja itajumuisha Watu Watano. Ndugu Kazimoto aliendelea kufafanu kuwa huduma za kujiandikisha zitatolewa katika Ofisi zote za Watendaji wa Mitaa zilizopo Mji wa Korogwe.
Kwa upande mwengine, Wananchi walijitokeza katika uzinduzi wa Kampeni ya Bima ya Afya ya CHF iliyoboreshwa walishukukuru Serikali na Wadau wa Afya kwaujumla kwa Kuwapatia huduma ya Bima ya Afya kwa gharama nafuu.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.