Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Korogwe amekutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa
Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bwana Kasimu Kaoneka amekutana na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa pamoja na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa lengo la kufahamiana vilevile kuelimishana kuhusu kanuni na sheria za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi novemba mwaka huu.
Mkutano huo ulifanyika septemba 18, katika ukumbi wa mikutano wa wa Halmashauri ya Mji Korogwe. Katika mkutano huo Bwana Kaoneka aliambatana na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Bwana Charles Mtali wote kwa pamoja walitoa elimu ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku wakisisitiza umuhimu wa kufuatwa kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepukana na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.
Bwana Mtali aliendelea kusema kuwa uchaguzi huu utahusisha Vijiji pamoja na Mitaa katika wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe yenye mitaa 22 na vitongoji 35 ambapo kutakuwa na jumla ya vituo 62 vya kuandikisha na kupiga kura. Aliainisha eneo la Mitaa litakuwa lina vituo 27 na eneo la Vijiji litakuwa na vituo 35.
Kwa upande mwingine Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ambaye pia ni msimsmizi msaidizi wa uchaguzi Ndugu Magdalena John, amewasishi viongozI wa vyama vya siasa na wasimamizi wa uchaguzi kutumia kanuni na sheria za uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuepuka kupotoshwa na watu wengine.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.