RUWASA watoa mafunzo ya usimamizi wa miradi ya maji
Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wametoa mafunzo ya usimsmizi wa miradi ya maji kwa jumuiya za watumiaji maji Wilaya ya Korogwe. Mafunzo yalishirikisha jumuia takribani kumi (10) kutoka Halmashauri zote mbili zilizopo Wilaya ya Korogwe. Mafunzo hayo yalitolewa Februari 27, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzia mafunzo hayo Mhandisi Tupa Willium ambaye ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Korogwe alisema “lengo la mafunzo haya ya usimamizi wa miradi ya maji ni kuwajengea uwezo watumiaji wa maji waweze kusimamia vizuri miradi ya maji katika jumuia zao” Mhandisi Tupa aliendelea kufafanua kuwa RUWASA pamoja na jumuia ya watumiaja maji ni vyema kushirikiana kwa pamoja katika miradi ya maji ili iweze kunufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.
Nae Ndugu David Mpumilwa ambaye ni muwezeshaji wa mafunzo haya kutoka RUWASA alitoa ushauri kwa kusema “ ni muhimu wananchi wajiepushe na matumizi ya maji yasiyo sahihi ili kuepuka gharama kubwa za malipo ” Kwa upande mwingine Ndugu Hassani Mkindi ambaye ni mwanajumuia kutoka Kata ya Mazinde aliishukuru RUWASA kwa kuwapatia mafunzo ya usimamizi ya miradi ya maji. Ndugu Mkindi pia alitoa ushauri wa RUWASA kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kulinda vyanzo vya maji ili vidumu kwa kizazi kilichopo na kijacho.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.