Shule ya Sekondari ya Korogwe Girls yasafirisha wanafunzi
Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Korogwe Girls iliyopo Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga umekamilisha mchakato wa kusafirisha wanafunzi wote baada ya tamko la Serikali la Machi 17, mwaka huu kutaka shule zote zifungwe kuanzia shule za awali hadi Kidato cha sita kwa lengo la kupambana na maradhi ya Corona.
Akizungumzia mchakato huo, Bi. Annisia Mauka ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Korogwe Girls alisema “ tumekamilisha mchakato wa kusafirisha wanafunzi wote kurudi nyumbani”. Bi. Mauka aliendele kufafanua kuwa mchakato wa kusafirisha wanafunzi takribani mia tisa sabini na saba (977) kuelekea mikoa mbalimbali hapa nchini ulichukua siku tatu kuanzia Jumatano hadi leo Ijumaa kutokana na changamoto ya usafiri.
Katika hatua nyingine Bi. Mauka ametoa ushauri kwa Shirika la Reli Tanzani ambalo linafanya safari zake Kati ya Dar es salaam na Arusha kuchangamkia fursa za kusafirisha wanafunzi wanaoelekea Mikoa ya Kanda ya Pwani pamoja na Kanda ya Kaskazini. Katika kipindi cha likizo kuna changamoto kubwa ya usafiri hivyo shirika la reli Tanzania linaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi.
Nae Mwl. Boniface Kinyemi kutoka shule ya Sekondari ya Korogwe Girls ambaye anaratibu mchakato wa kusafirisha wanafunzi hapo shuleni alisema “ taratibu zote za safari zinakwenda vyema na mpaka kufikia leo Ijuma wanafunzi wote watafanikiwa kwenda nyumbani”. Kwa upande mwingine wanafunzi walitoa shukrani kwa uongozi wa shule kwa jitihada walizofanya katika kuhakikisha wanapata usafiri wa kurudi nyumbani.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.