Wanafunzi 1343 wajiunga darasa la kwanza katika Mji wa Korogwe
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imefanikisha kuandikishaji jumla ya wanafunzi 1343 wanaotarajia kujiunga na darasa la kwanza kwa mwaka 2021. Wavulana walioandikishwa ni 672 na Wasichana ni 671 ambapo wastani wake ni sawa na Wavulana asilimia 63 na Wasichana ni asilimia 65. Mchakato huo wa uandikishaji ulianza Oktoba 1, mwaka 2020 katika shule zote za Serikali katika Mji wa Korogwe na unatarajiwa kukamilika Machi 31, mwaka huu.
“Halmashauri ya Mji wa Korogwe tunatarajia kusajili jumla ya wanafunzi 2109 kwa ajili ya darasa la kwanza kwa mwaka 2021” alisema Ndugu Meinrad Komba ambaye ni Afisa Elimu Takwimu katika Idara ya Msingi. Ndugu Komba alifafanua kuwa uandikishaji wa wanafunzi hao 2109 unajumlisha Wavulana 1073 pamoja na Wasichana 1036.
“Katika shule yetu wazazi wana muitikio mkubwa katika kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza” alisema Mwl. Hamisi Mketo ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Manundu Mazoezi wakati wa ufuatiliaji wa mchakato wa uandikishaji wa darasa la kwanza kwa mwaka 2021. Kwa upande mwingine Wazazi walioshiriki katika mchakato wa uandikishaji wa wanafunzi waliishukuru Serikali kwa kuweka utaratibu mzuri wa uandikishaji wa wanafunzi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.