Wanawake wa mji wa korogwe waadhimisha siku ya wanawake duniani
Wanawake katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe wameadhimisha siku ya wanawake duniani, siku ambayo huadhimishwa dunia nzima ifikapo Machi 8, ya kila mwaka. Maadhimisho ya mwaka huu alifanyika katika eneo la Soko la Kilole lililopo jirani na Kituo kikubwa cha mabasi cha Kilole.
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikua Mh. Kissa Kasongwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe. Wakati wa hotuba Mh. Kasongwa aliwapongeza wanawake kwa jidihada wanazofanya katika kujiletea maendeleo na alisema “ Serikali itahakikisha Halmashauri inatenga fedha asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya wanawake ili waweze kujiajiri kupitia shuighuli mabalimbali za ujasiriamali.”
Akizungumzia maadhimisho hayo ndugu Charity Sichoma ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe alisema kuwa siku ya wanawake duniani ni siku ambayo huadhimishwa kila mwaka kwa lengo kuelimisha wanawake kuhusu kupinga vitendo vya unyanyasaji, unyonyaji na ukandamizaji kwa wanawake kijinsia, kiuchumi, kiutamaduni na kiutawala. Kauli mbiu ya mwaka mwaka 2020 ni “ kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na badae”
Kwa upande mwingine Bi. Naomi Frederick kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa aliwaasa wanawake kujiepusha na rushwa ya ngono wakati kwakuomba kazi, kipindi cha uchaguzi au kwa ajili ya kupewa upendeleo wa aina yoyote. Nae Bi. Jane Samkieli kutoka kikundi cha Agape kinachojishughulisha na kazi za mikono alisema “wanawake tunafuraha kubwa kukutana pamoja katika siku ya wanawake duniani, siku ya leo itatusaidia kubadilishana mawazo ya namna ya kujiajiri pamoja na kutafuta fursa za kiuchumi”
Katika Mji wa Korogwe maadhimisho hayo yaliambatana na utolewaji wa huduma za afya pamoja na matukio mbalimbali kama za vile upimaji wa kansa ya mlango wa kizazi pamoja na kansa ya matiti, chanjo ya kansa ya matiti kwa wasichana pamoja na kufanya vipimo vya virusi vya ukimwi (HIV) na ushauri nasaha. Pia kulitolewa elimu ya kupambana na rushwa, elimu ya ndoa, miradhi na usia vilevile upandaji wa miti ya aina mbalimbali.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.