Watumishi wa mji wa korogwe wapata mafunzo ya kupambana na ukimwi
Halmashauri ya Mji wa Korogwe imetoa mafunzo ya kujikinga na maradhi ya ukimwi kwa watumishi wa umma pamoja na wazee wanaoishi katika Mji wa Korogwe. Mafunzo haya yalitolewa novemba 27. Mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzia mafunzo haya Dkt. Elizabeth Nyema ambaya ni Mganga mkuu wa Halmashuri ya Mji wa Korogwe ambaye pia anamuakilisha Mkurugenzi alisema lengo la mafumzo haya ni kuwakumbusha watumishi wa umma pamoja na wazee wa Mji wa Korogwe kufahamu kuwa ugonjwa wa ukimwi bado upo na nijanga la kitaifa hivyo wasiuchukulie poa sababu unangamizi nguvu kazi ambao ni tegemeo katika maendeleo ya familia na nchi kwa ujumla.
Nae ndugu Farasi Isihaka ambaye ni muakilishi wa shirika la AFRIWAG linalojihusisha na mapambano dhidi ya ukimwi alisema wazazi hususani wazee wanatakiwa kuwa na tahadhari kubwa wakati wa kumhudumia mgonjwa aliyeathirika na maradhi ya ukimwi ili wanapouguza wasipate maambukizi. Ndugu Isihaka aliendelea kusema kuwa ni vyema wanachi kupiga vita mila na desturi za kurithi wajane ili kujiepusha na maambukizi mapya ya ukimwi.
Kwa upande mwingine Bi.Jackline Mritha ambaye ni mshiriki wa mafunzo alitoa ushauri kwa wawezeshaji wa mafunzo kuhakikisha wanawafikia wananchi wa vijijini na kuwafundisha namna ya kupambana na ugojwa wa ukimwi pamoja na kumhudumia mgonjwa wa ukimwi.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.