Wenyeviti wa Mji wa Korogwe waapishwa baada ya CCM kushinda 100%
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Wilaya ya Korogwe Mh. Nemes Mombury amewapisha Wenyeviti pamoja na Wajumbe wa mitaa na vijiji katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe baada ya kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24, mwaka huu. Kiapo hiki kilifanyika Novemba 28, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Wakati wa kiapo Mh. Mombury alitoa nasaha kwa viongozi wote wa mitaa na vijiji kuwahudumia wanachi bila ya kujali itikadi za vyama vya siasa. Mh. Mombury aliongeza kusema kuwa wananchi wanahitaji kupata maendeleo na sio mvutano wa vyama vya siasa. Pia aliwasisitiza viongozi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha wananchi wako salama wakati wanafanya shughuli zao za maendeleo katika jamii.
Nae Bwana Felix Pima ambaye ni mwenyekiti wa Mtaa wa Mtonga alisema anafuraha kuwa kupata ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu. Bwana Pima aliongeza kusema kuwa amejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wa mtonga wanapata maendeleo hususani huduma za jamii kwa kushirikiana na idara za husika. Kwa upande mwindine Bi. Mwanaidi Mussa ambaye ni Mjumbe wa mtaa wa Memba amesema ushindi wake ni zawadi kwa wanachi wa memba hivyo atawapa ushirikiano wa kutosha katika kuleta maendeleo.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.