Wilaya ya Korogwe yaadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani
Wafanyakazi kutoka Sekta za Umma pamoja na Binafsi Wilayani Korogwe wameadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani. Siku ambayo huadhimishwa Duniani kote ifikapo Mei 01 ya kila mwaka. Kauli Mbiu ya mwaka huu ni Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee” Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Chuo Cha Ualimu Korogwe (Korogwe TTC) huku Mgeni rasmi akiwa Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.
“Katibu Tawala nenda kwa Wakurugezi ukasimamie maslahi ya watumishi” alisema Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe wakati akizungumza na watumishi kutoka Sekta za Umma na Binafsi walioshiriki siku ya Maadhimisho ya Mei 01 mwaka huu. Mhe. Kasongwa alifafanua kuwa Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan iko bega kwa bega na watumishi na itahakikisha kila mtumishi anapata maslahi bora ili kufikia malengo yake.
“Wafanyakazi wajiunge kwa wingi kwenye vyama vya wafanyakazi ili kua na sauti ya pamoja katika kutetea maslahi ya wafanyakazi”. Alisema Ndugu Mohamed Semkamba ambaya ni Mwenyekiti wa Shirikisho huru la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Wilaya ya Korogwe. Nae Bi. Pili Mdoe ambaye ni Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilayani Korogwe aliwasilisha risala kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe huku alitoa msisitizo kwakusema “changamoto kubwa inayowakumba watumishi ni kuchelewa kupanda madaraja (mishahara) kwa wakati”.
Kwa upande mwengine, Wafanyakazi kutoka Vyama mbalimbali kama vile TALGWU, CWT, TUGHE, TUICO pamoja na Chama cha TPAWU walitoa shukrani kwa Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi na Serikali kwa ujumla kwa maandalizi mazuri ya Maadhimishi hayo. Katika Maadhimisho ya Mwaka huu Watumishi pia walishiriki katika michezo mbalimbali kama vile mchezo wa Mpira wa miguu pamoja na Mpira wa mikono (Rede). Michezo mingine ni pamoja na Kuruka Kamba, Kukuna Nazi pamoja na Mbio za Kukimbia na Magunia.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.