Wilaya ya Korogwe yapata mafunzo ya ufugaji wa nyuki
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Mh. Edmund Mndolwa amefungua mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa Mkoa wa Tanga. Mafunzo ambayo pia yalihudhuriwa na Mh. Kissa Kasongwa ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Korogwe pamoja na Wakurugenzi kutoka Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Korogwe. mafunzo hayo yalizinduliwa Machi 16, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Akizungumzia mafunzo hayo Mh. Edmund Mndolwa ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Tanzania alisema “lengo la mafunzo haya ni kuhamasisha ufugaji nyuki kwa vijana na vikundi kwa ujumla ili wajikwamue kiuchumi”. Mh. Mndolwa alifafanua kuwa kwa sasa ufugaji wa nyuki unalipa na ni muda muafaka kwa vijana kujiajiri kupitia ufugaji wa nyuki
Katika hatua nyingine Mh. Mndolwa amewahakikishia wafugaji wa nyuki kuwa kuna soko la kutosha la bidhaa za nyuki ndani na nje ya nchi. Alitoa ushauri kwa wafugaji watumie mizinga ya kisasa ili wapate asali ya kutosha pamoja na bidhaa nyingine za nyuki. Pia alitoa maelekezo kwa Jumuiya ya wazazi katika kila Wilaya watenge hekari moja kwa ajili ya ufugaji wa nyuki.
Nae Bi. Groria Joseph mwezeshaji wa mafuzo kutoka chuo cha International Beekiping Openi School kilichopo Mkoani Singida alisema “ ni vyema vijana tukachangamkia fursa ya ufugaji wa nyuki ili kuongeza kipato pamoja na kupata lishe bora kwa ajili ya afya zetu” Bi. Groria alifafanua kuwa ufugaji wa nyuki una tija kubwa kwa mfugaji ikiwepo kupata bidhaa kama vile asali, nta, pamoja na gundi ya nyuki. Bidhaa nyingine ni sumu ya nyuki, supu ya nyuki, maziwa ya nyuki na chavua.
Kwa upande mwingine Bi. Rehema Kazenga ambaye ni mshiriki wa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kutoka Mji wa Korogwe aliishukuru Jumuia ya Wazazi Tanzania kwa kuandaa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa kuwa mafunzo haya yatawasaidia vijana pamoja na vikundi vyengine kujiajiri kupitia ufugaji wa nyuki.
Korogwe Tanga Tanzania
S.L.P: 615 Korogwe
Simu: 0272650050
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@korogwetc.go.tz
Copyright©2018 Korogwe Town Council. All rights reserved.